Mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza 2014/15,Chelsea wameanza msimu wa 2015/16 kwa kusua sua hali iliyopelekea kuwepo na tetesi kua kocha Jose Mourihno angefukuzwa Stamford bridge. Leo nakuchambulia sababu zinazoifanya timu ya Chelsea kufanya vibaya msimu huu.
1. Beki wa Kulia
Chelsea imekua na tatizo katika upande wa beki wa kulia nafasi ambayo mkongwe Ivanovic anacheza,Ivanovic ameshindwa kua kwenye fomu msimu huu kwa wanaofuatilia mechi kwa njia ya TV watakua mashahidi wangu kwani ivanovic amekua anapitika kirahisi msimu huu na pia amesababisha makosa mengi yaliyopelekea Chelsea kufungwa.
2. Kiungo(Midfielders)
Ukija upande wa kiungo napo pamekua na tatizo pengine zaidi kuliko upande wa ulinzi, Cesc Fabregas na Nemanja Matic wameshindwa kuendelea na kiwango chao kama msimu uliopita kitu kinachopelekea washambuliaji kukosa mipira mbele pia kitu kinachowapatia wapinzani muda mwingi wa kukaa na mpira na kufanya mashambulizi.
3.Eden Hazard
Bila ubishi Hazard ndiye Messi na Ronaldo wa Chelsea ,kuanza vibaya kwa Hazard msimu huu kimechangia asilimia kubwa kwa Chelsea kufanya vibaya msimu huu kutokana na kushindwa kua na mashambulizi makali ya kumsumbua adui.
4. Kukosekana kwa Diego Costa
Kukosekana kwa Diego Costa kwenye mechi kadhaa kumewafanya Chelsea kutokua na mshambuliaji mwenye kuogopwa na mabeki hata kwa kuwasumbua .


No comments:
Post a Comment