Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Wakati Diego Costa akiifungia Chelsea goli la saba msimu huu,Chelsea walikua kwenye kiwango cha hali ya juu leo wakiweza kumiliki mchezo kwa dakika 90 zote. na haya ni baadhi ya mambo tuliyo yaona leo.
1.Chelsea wameumudu vizuri mfumo mpya wa Antonio Conte 3-4-3.

Chelsea walionyesha mchezo mbaya sana dhidi ya Arsenal mechi ya mwezi uliopita ndipo kocha Antonio Conte akaamua kurudi kwenye mfumo wake uliompa mafanikio katika klabu ya Juventus wa 3-4-3 huku mabeki wa watatu wakikaa kati na akiwatumia Alonso na Azpilcueta kama mabeki wa pembeni wanaopanda kushambulia kitu ambacho wote wamekimudu vizuri bila shaka walioangali mpira wameonajinsi Chelsea walivyokua wakipiga counter attack hatari.
2.Victor Moses ana nafasi ya kua nyota wa kutegemewa pia.



Winga huyo wa Nigeria alihamia Chelsea huku mashabiki wakiaamini kua nyota huyo ataanza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza ila alishindwa kufanya vizuri na alitolewa kwa mkopo katika klabu kadhaa ila tangu Conte achukue timu Victor Moses ameonyesha matumaini kua anaweza kua nyota wa kutegemewa huko mbeleni japo kwa sasa anashindwa kuumudu mchezo kwa dakika 90.
3.Conte ameonyesha mwanga kwa wachezaji wanaochipukia




Klabu ya Chelsea imekua ikisifiwa kwa kuwa na wachezaji wadogo wengi wenye viwango vya hali ya juu ila imekua ikikosolewa kwa kushindwa kuwatumia vijana hao ambao baadaye huondoka na kwenda kufanya vizuri timu nyingine ila hilo linaweza kufikia mwisho kwani kocha Conte ameonyesha nia ya kuwatumia vijana wadogo kwani kwa leo tuu aliweza kuwapa nafasi Nathaniel Chalobah aliyechukua nafasi ya Pedro,Ruben Loftus-Cheek aliyechukua nafasi ya Eden Hazard na Ola Aina aliyechukua nafasi ya Victor Moses,Nathaniel Chalobah hakumuangusha bosi wake kwani alitoa pasi nzuri iliyowekwa nyavuni na Victor Moses.

4.N'golo Kante ni zaidi ya tulivyowahi kumjua(Ni nyota asiyepewa heshima ya kutosha).

Mashabiki wa Chelsea wamemtunga N'golo Kante jina la Jenerali ni kweli na anastahili kwani kila mechi andhidi kutuonyesha yeye ni zaidi ya mechi iliyopita uwezo wake wa kukaba kutibua mashambulizi na kufanya counter attack,amekua akitumia vizuru speed yake na Kante ndio mchezaji bora wa mechi ya leo.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib