Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

3-4-3Antonio ConteChelseaConte press conferenceWillian

Kikao na waandishi wa habari vitu alivyosema kocha Antonio Conte kuhusu mechi ya leo na kuhusu Willian.



Kocha Antonio Conte hakuisha kukusifia kikosi chake leo baada ya kuonyesha kiwango cha juu dhidi ya mabingwa watetezi Leicester na kuibuka na magoli matatu kwa bila Conte alianza kuongea kama ifuatavyo.
"Leo nina furaha kwa kua nimeona vile vyote tulivyokua tukivifanyia mazoezi kwa nzima vikizaa matunda ila yote najisikia faraja kwa wachezaji kwani mkifanya mazoezi kwa kiwango kikubwa mnategemea kuona matokeo mazuri"
"Kipindi cha kwanza tulionyesha mchezo mzuri wa kushambulia kwa kasi tumepiga pasi nzuri na tumeweza kuwatafuta washamuliaji kwa mipira mingi ya pembeni ila tulikua tukitafuta mpira kwa nguvu kila tunapopoteza"
Akiulizwa kuhusu mfumo wake mpya wa 3-4-3
"Nimebadilisha mfumo katika mechi mbili za mwisho kwa sababu unapofika katika timu unakuta wana mfumo ambao wameuzoea hivyo unahitaji muda sahihi kubadilisha mfumo wao na kuweka wa kwako"
Alipoulizwa sababu ya mshambuliaji Diego Costa kuonyesha ishara ya kua anataka abadilishwe
"Conte amesema kua Diego Costa tayaria ana kadi nne za njano na kama angeonyeshwa kadi moja tu ya njano leo ina maana angekosa mechi inayofuata hivyo mapenzi yake kwa timu yalimfanya aombe kubadilishwa ili aweze kucheza mechi inayokuja"
Conte pia alimpa pongezi Victor Moses
alisema "Wakati nafika Chelsea niliwaambia kua ningependa kumuona Victor Moses kwenye mechi za kujiandaa na msimu kwa sababu nilijua ana umuhimu mkubwa nimekua nikimfuatila Victor Moses kwa muda mrefu anacheza vizuri sana kama beki mshambuliaji ana umakini mkubwa sana kwenye ulinzi na anapanda kushambulia anapopata nafasi.
Conte alimaliza kwa kusema Ushindi wa leo ni maalumu kwa ajili ya mwenzetu Willian aliyefiwa na Mama yake tunajua ni kipindi cha majonzi kwake na kwetu hivyo tunautoa ushindi huu kwake.

Asante kwa kua nasi usisahau kutembelea tena kesho upate habari nyingine.Please Share na marafiki zako .Asante Sana.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib