Climb the mountains
Antonio ConteChelseaCourtoisDiego CostaThibaut Courtois
Baada ya wote kutaka kuondoka msimu uliopita sasa Diego Costa na Thibaut Courtois wasema wako tayari kusaini mikataba mipya.
Dirisha la usajili lililofungwa mwezi mwezi wa nane mashabiki wa Chelsea walikua hna hofu ya kuwapoteza nyota wao yani Diego Costa na Thibaut Courtois. Costa alikua akihitajika na klabu yake ya zamani Atletico Madrid huku Thibaut Courtois alikua akihitajika na klabu kubwa barani ulaya na aliweka wazi kua anataka kurudi nchini Hispania. Taarifa ndani ya klabu zinasema wachezaji hao walikutana na kocha mkuu wa Chelsea Antonio Conte na aliwaweka wazi kua anawahitaji katika kikosi chake lakini pia aliwaeleza mipango yake ya kuifanya Chelsea kua timu tishio tena na wao ni sehemu kubwa ya huo mpango na hivyo aliwasihi kukubali mikataba mipya ili waweze kufanya kazi pamoja. Kama mikataba hiyo ikisainiwa basi itakua ngumu kwa nyota hao kuondoka darajani hivi karibuni.
Tags: Antonio Conte
, Chelsea
, Courtois
, Diego Costa
, Thibaut Courtois
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment