Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Antonio ConteChelseaswansea

Antonio Conte: Nina timu inayostahili kuongoza ligi kuu ya Uingereza.


Kocha wa Chelsea Antonio Conte hakusita kuisifia timu yake baada ya kupita mtihani wa timu ngumu inayopigania kutoshuka daraja ya Swansea na kusema ana timu ambayo inastahili kuongoza ligi kuu ya Uingereza , Conte alishuhudia vijana wake wakiicharaza timu ya Swansea magoli matatu kwa moja na kujikita usukani mwa ligi kwa tofauti ya alama 11 huku wakiwa na pointi 63 katika mechi 26, tukiaangalia kumbukumbu inaonyesha mabingwa wa Ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita Leicester City walichukua ligi hiyo kwa pointi 60 ambazo Chelsea amezifikia na kuzipita msimu huu kitu kinachoonyosha msimu uliopita haukua mbaya kwa Chelsea tuu bali hata timu nyingine kubwa. Pia Conte alisema 'Leo nimeata majibu sahihi kutoka kwa wachezaji wangu unapocheza mechi na timu zenye shinikizo kubwa kama Swansea inabidi ujibu kwa usahihi kitu walichofanya wachezaji wangu' akimaanisha wacheaji walijituma kuongeza magoli mawili licha ya kua Swansea walikua wakijaribu kuwashambulia.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib