Climb the mountains
Chelsea LegendChelsealeading goal ScorerFrank LampardLampard farewellLampard retire
Frank Lampard: Nisingeweza kufanya bila nyinyi. Maneno ambayo Lampard aliwaambia mashabiki wa Chelsea baada ya kupewa nafasi ya kuwaaga.
Jana Chelsea ilimpa mkongwe wao nafasi ya kuwaaga mashabiki vizuri baada ya kushindwa kufanya hivyo kipindi alichoondoka. Wakati wa muda wa mapumziko kiungo huyo raia wa Uingereza ambaye ametangaza rasmi kustaafu soka aliingia Uwanjani na kuanza kusema "Sikupata nafasi nzuri ya kuwaaga wakati naondoka Chelsea ila nataka kuishukuru klabu leo kwa kunipa nafasi ya kufanya hivo na la muhimu zaidi nataka kuwashukuru sana nyote,asante kwa kumbukumbu na nyakati muhimu zote ambazo bado nazikumbuka mpaka leo nisingeweza kufanya bila nyie,tusingeweza kufanya bila nyie asanteni sana" Lampard ni mchezaji aliyewahi kuicheza Chelsea ambaye ana magoli mengi zaidi kuliko mchezaji yoyte yule akiwa ameifungia Chelsea magoli 211 na akiwa amecheza mechi 648. Pamoja na Lampard kustaafu ameanza mafunzo ya ukocha akipata shule hiyo kutoka Academy ya Chelsea akiwa pamoja na Ashley Cole pamoja na John Terry.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





No comments:
Post a Comment