Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaDiego CostaPedroQuater FinalsWolverhampton

Chelsea waipiga Wolverhampton 2 bila,wafuzu robo fainali.


Klabu ya Chelsea jana ilifanikiwa kuwafunga Wolverhampot kwa magoli mawili kwa bila magoli hayo yakifungwa na Pedro aliyefunga goli la kwanza kwa kichwa na goli la pili likifungwa na Diego Costa dakika za lala salama,hata hivyo haikiuwa kazi rahisi kwa Chelsea kwani katika kipindi cha kwanza Wolves nao walicheza mpira wa kujilinda na kujaribu kushambulia. Katika mechi ya jana pia mkongwe John Terry alianza na kufanya kua mechi yake ya tatu msimu huu kitu ambacho kimeanza kuashiria huenda Terry asiwe mchezaji wa Chelsea msimu ujao kwani amekua akipata namba kwa nadra sana msimu huu

Alama za Wachezaji wa Chelsea



Begovic - 6 Ilikua mechi yake ya pili bila kuruhusu goli msimu huu.
Zouma -7 Aliweza kuipata mipira mingi ya juu.
Terry -7 Alikiongoza kikosi vizuri kama kawaida yake ila miguu imeanza kuchoka ni muda sahihi kwake kutundika daruga
Ake -7 Aligeuzwa kama udhaifu wa Chelsea ila Pedro alikua akimsaidia
Moses -6 Alimiliki mpira vizuri ila mara nyingi alishibdwa kuwapita mabeki wa pembeni
Chalobah -5 Hakua na mchezo mzuri kutokucheza mara kwa mara inaweza kua sababu
Fabregas -6 Alikosa nafasi za wazi kwenye pasi za mwisho
Pedro -6 Alipata kadi ya njano lakini alikua na mchezo mzuri na kutupatia goli la kuongoza
Willian- 8 Alielewana vizuri na Pedro alikua mwiba kwa walinzi wa Wolves
Costa- 8 Alikua mchezaji bora wa mechi alichezewa rafu nyingi na alistaihili kupata goli kwenye mechi ya jana
Hazard -5 Alikua kwenye kiwango kibaya kama msimu uliopita alishindwa kuonyesha cheche zozote

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib