Climb the mountains
ChelseaChelsea Vs SwanseaFabregasFabregas 300 matchesSpain
Fabregas afikisha mechi ya 300 ligi kuu ya Uingereza,asema hana mpango wa kuondoka Chelsea msimu ujao.
Tunaweza kusema jana ilikua siku njema kwa Cesc Fabregas kwani alikua anatimiza mechi yake ya 300 tangu aanze kucheza ligi kuu ya Uingereza na kuvunja rekodi ya kua mchezaji wa kwanza kutoka nchini Hispania kufikia idadi hiyo ya mechi. Jana Fabregas ndiye alikua mcheaji bora wa mechi (Man of the match) akifunga goli moja na kutengeneza goli pia alikimudu kiungo vizuri hasa katika kutengeneza mashambulizi kwa jana Chelsea ilicheza mpira wa kushambulia zaidi kuliko mechi kadhaa za nyuma. Pamoja na hayo Cesc aliweka wazi kua hafikirii wala hana mpango kuondoka Chelsea msimu ujao na anaamini atabaki klabuni hapo kwa muda mrefu sana.
Tags: Chelsea
, Chelsea Vs Swansea
, Fabregas
, Fabregas 300 matches
, Spain
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment