Climb the mountains
ChelseaShayShay - Thibaut CourtoisThibaut Courtois
Msanii wa Ufaransa aupatia wimbo wake jina la kipa wa Chelsea Thibaut Courtois,ila akana na kusema ni nyimbo tuu hakuna uhusiano wowote kati yao.
Kipa wa Chelsea ameingia kwenye headlines barani Ulaya baada ya msanii wa Ufaransa mdada anayejiita Shay Raunchy kuachia wimbo wake mpya ambao ameuita Thibaut Courtois tunaweza kusema ameamua kuupa jina la kipa wa Chelsea wimbo wake huo mpya ambao mpaka sasa umetazamwa na watu 880,550 kwenye chaneli yake ya Vevo. Thibaut hajaonekana kwenye video hiyo ila maneno yaliyoimbwa kwenye wimbo huo yanamlenga moja kwa moja kipa huyo. Alipoulizwa kuhusu wimbo huo msanii Shay alisema ameuita Thibaut Courtois kwa sababu amevutiwa na jina la mchezaji huyo hajamchagua sababu ni mchezaji mpira maarufu na hajawahi kukutana nae pia amesema wimbo wake unahusu kuumizwa kwenye mahusiano hivyo ameimba akimaanisha atajisikia mwenye amani kupata mtu mtunzaji(Keeper) kama Thibaut akimaanisha kipa huyo anavyolilinda goli lake uwanjani.
Tags: Chelsea
, Shay
, Shay - Thibaut Courtois
, Thibaut Courtois
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment