Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaCobhamConteMaurizio Sarri

Maurizio Sarri kutua London muda wowote,aamua kuweka makazi yake Cobham kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea.


Wakati mashabiki wa Chelsea wakiwa bado hawana kauli moja kuhusu ujio wa kocha mpya,kocha anayetajwa kuchukua nafasi ya Antonio Conte anatarajiwa kutua London muda wowote kuanzia leo. Maurizio Sarri kutoka klabu ya Napoli amekua akihusishwa muda mrefu kuchukua mikoba Chelsea na hivyo inaonekana yanakwenda kutimia. Katika jambo ambalo sio kawaida kocha huyo amechagua kuweka makazi yake katika kiwanja cha Cobham kinachotumika kwa ajili ya mazoezi na wachezaji wa Chelsea na inasemekana tayari Chelsea wamemuandalia nyumba ya hadi yake kiwanjani hapo. Mashabiki wa Chelsea wamekua na mitazamo tofauti mitandaoni wengine wakionyesha kumuunga mkono Conte wengine wakisema Chelsea inahitaji kocha mwenye CV kubwa zaidi ya Sarri,je nini maoni yako unadhani Sarri atafanikiwa katika kikosi cha Chelsea?

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib