Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Andreas ChristensenBarcelonaBiographyChelsea

Mfahamu Andreas Christensen kinda wa Chelsea anayenyatiwa na klabu kubwa ulaya ikiwemo Barcelona

Andreas Christensen, ni raia wa Denmark alizaliwa 10/04/1996. Christensen anacheza nafasi ya beki wa kati, alijiunga na Kikosi cha watoto cha  Chelsea akitokea Brondby baada ya kuonyesha uwezo na ufundi mkubwa alipata namba kwenye kikosi cha under 18 na baadae under 21 na hivo kuweza kukisaidi kikosi cha under 21 kushinda UEFA Youth league. Baada ya kiwango kizuri alipewa mkataba rasmi mwaka 2013.
Mafanikio.
Mwaka 2015 disemba katika tuzo zinazofanyika nchini kwao kila mwisho wa mwaka  alichaguliwa kua mchezaji mdogo anaye chipukia mwenye kipaji cha hali ya juu (Danish Talent of the Year award) tuzo hiyo hutolewa kwa mchezaji bora anayechipukia anaeyecheza mpira ulaya.  Ila mwaka 2015 huo huo ilitangazwa kua anaenda Borussia Monchengladbach kwa mkopo wa miaka miwili. Tangu ajiunge na klabu hiyo kwa mkopo amefanikiwa kuteka macho ya vilabu vikubwa vya ulaya kwa uwezo mkubwa aliouonyesha kwenye ligi ya Bundesiliga,amekua akihusishwa na klabu ya Barcelona, Arsenal na Manchester united,hata hivo Chelsea wanahisi atakua mbala mzuri kurithi mikoba ya mkongwe John Terry. Na huyo ndo Andreas Christensen

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib