Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

2015/2016Alvaro MorataCheleachelsea tanzaniaEdinson CavanilukakuRumorsTetesi za usajili

Lukaku Paundi Mln75 Morata Paundi Mln 67,Cavani Paundi Mln 42-Kwa mtazamo wako tumsajili nani kati ya hawa?

Wakati klabu ya Chelsea wakiwa bado wanatafuta mshambuliaji mwingine,mpaka sasa wanahusishwa na washambuliaji hawa watatu Lukaku,Morata na Cavani. Kiukweli waxhezaji hawa hawana haja ya kudhibitisha uwezo wao tena kwa sababu tumeshawaona ila wewe kama shabiki wa Chelsea unadhani yupi kati ya hao watafaa? Si mara ya kwanza Chelsea kutaka kumsajili Cavani, walishajaribu kufanya hivo miaka iliyopita ila Cavani aliamua kwenda PSG.

Alvaro Morata miaka 22,

Madrid wanataka kiasi cha paundi milioni 67 ili kumuachia mshambuliaji huyo aliyefanya vizuri akiwa na klabu ya Juventus nchini Italia, kama Chelsea wataamua kumsajili Morata watakua wamewekeza kwani Morata bado ana umri mdogo tutakua tumewekeza.

Romelu Lukaku miaka
Romelu Lukaku si mgeni kwenye klabu ya Chelsea kwani alihamia Chelsea akiwa bado ana miaka 18 tuu hakuweza kufanya vizuri sana ila baadae aliomba kuondoka na kuruhusiwa alijiunga na klabu ya Everton na kufanikiwa kung'aa sana kiasi cha kua moja ya washambuliaji waliofukuzia tuzo ya mfungaji bora wa msimu kwa mtazamo wangu kwa kua tumeshamsajili Mitch Batshuayi ni bora Chelsea wakaachana na Lukaku kwani hawatofautiani sana staili ya uchezaji wao.

Edison Cavani
Hii si mara ya kwanza Chelsea tumehusishwa kumsajili Edsoni Cavani ila kitu kinacho fanya Chelsea wajaribu kumsajili mchezaji huyo mara kwa mara ni staili ya uchezaji wake wa kutumia nguvu na akili, tangu aende PSG amekua kama mbadala wa Zlatan Ibrahimovich ila amaekua akifanya vizuri kila anapopata nafasi kwa matazamo wangu kama tukimkosa Morata ni bora tumsajili Edson Cavani anatatupa kitu tofauti kwenye kikosi chetu pata picha kama siku kitaanza kikosi tukiwa na washambuliaji kama Hazard Willian Cuodrado huku Costa na Cavani wakiongoza mashambulizi?


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib