Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaChelsea Vs Arsenal

Ripoti ya mechi Arsenal Vs Chelsea (3-0)


Kwanza tujipe pole mashabiki wa Chelsea pili tuwapongeze kabu ya Arsenal kwa kufuta uteja ila kikubwa nataka nichambue kidogo mechi ya leo,makosa na nini tunachotakiwa kufanya.
1.Chelsea tunahitaji beki wa kiwango cha juu(World Class Defender)

Kwa mlioangalia mechi leo mtakubaliana na mimi kuwa Chelsea kwa sasa tunamatatizo upande wa ulinzi kwani leo Arsenal leo walikua wanatufanya wanavyotaka Gary Cahill leo aligeuzwa uchochoro na nadhani ndo mchezaji aliyecheza chini ya kiwango kuliko wachezaji wote maoni yangu ni kamati ya Usajili hawana budi kufanya usajili wa mabeki wawili wa kiwango cha hali ya juu.

2.Mpaka sasa hatujui ni viungo gani wanatakiwa kuanza kwenye mechi au walio kwenye kiwango kizuri.
 Nadhani ni kitu kisichofichika kua mpaka sasa hatujui nani aanze kati ya Cesc Fabregas,Oscar na Matic. Mpaka sasa kocha Antonio Conte hajui aanze na nani katika safu ya kiungo japo amekua akionyesha kumpendelea Oscar na kumuacha Cesc nje, tunahitaji kujua wachezaji gani wanapaswa kuanza kati ya Matic,Oscar na Fabregas.

3.Conte awape nafasi wachezaji wengine ili kuleta ushindani wa namba kwenye kikosi

Kwenye kikosi tuna wachezaji wengi wazuri ambao wanastahili kupewa nafasi ya kuonyesha viwango vyao pia inatubidi kuwarudisha baadhi ya wachezaji kwa mkopo,wachezaji kama Ola Aina,Nathaniel Chalobah na Andreas Christensen wanapaswa kupewa nafasi

4.Ni wakati wa bodi ya Chelsea kurudisha makali katika dirisha la usajili.

Nakumbuka wakati Peter Kenyon alipokua mkurugrnzi wa Chelsea upande wa usajili tulifanya vizuri sana katika usajili tuliweza kusajili wachezaji wazuri, sasa hivi tumekua hatufanyi vizuri kuwasajili wachezaji wa kiwango cha juu

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib