Haukua muda mzuri kwa Jose Mourinho kurejea darajani akiwa kama mpinzani kwani alikutana na kipigo kitakatifu cha bao nne kwa bila huku kikosi chake kikiwa kimejaa wachezaji nyota aliowanunua kwa fedha nyingi akiwemo mchezaji ghari zaid duniani Paul Pogba. Wakati Chelsea wakijipatia bao sekunde ya 30 tuu ya mchezo likifungwa na winga Pedro yafuatayo ni baadhi ya mambo tuliyoyaona kuhusu mechi ya jana.
1.Waliotuhumiwa kucheza chuni ya kiwango na kupelekea Mourinho afukuzwe wang'aa.
Msimu uliopita wakati klabu ya Chelsea ikiwa katika kiwango kibaya baadhi ya wachezaji walituhumiwa kucheza chini ya kiwango ili Jose afukuzwe wachezaji hao wakiwemo Eden Hazard na Diego Costa ila wote wameweza kurudi kwenye viwango vyao wakiwa chini ya Conte.
2.Pedro aanza kuonyesha matumaini mapya kwa Chelsea.
Wakati Chelsea wanamsajili winga Pedro walikua wamewazidi kete Manchester United kupata sahihi ya mchezaji huyo ila baada ya Pedro kutua darajani alishindwa kung'aa kama ilivyotarajiwa kitu kilichopelekea kutaka kuondoka mwezi January na August ila Conte hakutaka kumuuza msimu huu Pedro amekua na mchezo tofauti akionyesha kupanda kiwango kama alivyokua Barcelona.
3.Mfumo mpya wa Conte ndo nguzo kubwa ya Chelsea kuafanya vizuri.
baada ya kocha Conte kubadilisha mfumo Chelsea wamekua wakicheza mpira mzuri wa kuvutia na imekua nguzo kubwa sana ya Chelsea kufanya vizuri.
Kwa kumalizia Kocha Conte ameeonysha nia ya kumuibua nyota mwingine kutoka Chelsea Academy kwani ameendelea kumpa nafasi kiungo Nathaniel Chalobah na amekua akifanya vizuri pia N'golo Kante ameendelea kua mhimili muhumu wa timu.
Climb the mountains
Antonio ConteChelseaChelsea vs Manchester UnitedEden HazardJose Mourinho
Ripoti ya Mechi Chelsea vs Manchester United(4-0)
Tags: Antonio Conte
, Chelsea
, Chelsea vs Manchester United
, Eden Hazard
, Jose Mourinho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





No comments:
Post a Comment