Climb the mountains
Cesc FabregasChelsea Under 23JohnTerryKurt ZoumaMarco Van GinkelMitchy Batshuayi
Cesc Fabregas,John Terry,Kurt Zouma na Mitchy Batshuayi wacheza kikosi cha Chelsea Under 23 huku Conte akiwaangalia kama wapo tayari kuingia kikosi cha kwanza
Wakati Chelsea wakiendelea kufanya vizuri kwenye ligi wachezaji wengine waliowahi kutamba na kikosi cha kwanza na wanaotaka kupata namba ya kudumu kikosi cha kwanza wamendelea kujifua kwa nguvu kwenye kikosi cha Chelsea chini y miaka 23 ambapo pia huwajumuisha wachezaji kadhaa waliozidi miaka 23 kama sehemu ya kuwapa mafunzo wachezaji chipukizi,wikiendi hii wachezaji John Terry,Ces Fabregas,Mitchy Batshuayi na Kurt Zouma walikua kwenye kikosi kilichowavaa timu ya vijana ya Southampton ambapo Chelsea walifanikiwa kuibuka na Ushindi wa goli tatu Mitchy Batshuayi akifunga magoli mawili na mholanzi Marco Van Ginkel akifunga goli moja kukamilisha idadi ya magoli matatu.Wakati wachezaji hao wakicheza kocha wa Chelsea Antonio Conte alikua jukwaani kushuhudia mtanange huo kama sehemu ya majukumu yake pia kuangalia maendelea ya wachezaji wa akiba na wanaorudi kutoka majeruhi.
Tags: Cesc Fabregas
, Chelsea Under 23
, JohnTerry
, Kurt Zouma
, Marco Van Ginkel
, Mitchy Batshuayi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment