Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaJames RodriguezJanuary Transfersreal madrid

Baada ya James Rodriguez kuonekana akifuatilia Visa ubalozi wa Uingereza kunazidi kuwapa matumaini mashabiki wa Chelsea kua mchezaji huyo anakaribia kutua Stamford Bridge kwani Chelsea wameshatuma ofa kuomba kumsajili.


Aliyekua kinara wa mabao katika kombe la dunia 2014 James Rodriguez alionekana katika ubalozi wa Uingereza nchini Colombia akifuatilia Visa kitu kilichozidi kuongeza tetesi kua mchezaji huyo anaondoka klabu ya Madrid mwezi wa kwanza na kujiunga na moja ya klabu nchini Uingereza na klabu pekee ambayo mpaka sasa imeonyesha nia ya kumsajili ni klabu ya Chelsea ambao wameshatuma ofa, mshambuliaji huyo ambaye alifanya vizuri msimu wake wa kwanza alipojiunga na Real Madrid amejikuta akisugua benchi kwa muda mrefu. James mwenyewe alikarirwa akisema amepata ofa kutoka klabu mbali mbali na ana siku saba tuu za kuamua hatma yake. Chelsea wanataka kumsajili James kwa ajili ya kuziba nafasi ya Oscar anayetimukia nchini China.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib