Climb the mountains
#BradleyLoweyBradley LoweryChelseaNeuroblastomaSunderland
Bradley Lowery mtoto wa miaka 5,shabiki wa Sunderland aliyeamua kutumia siku za mwisho za uhai wake kuitumikia klabu aipendayo.
Bradley Lowery ni mtoto mwenye miaka mitano tuu anaye sumbuliwa na kansa ya Neuroblastoma. Bradley alipata kansa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka miwili tuu japo alifanikiwa kuishinda kansa na kupona ila kwa sasa imejirudia na imekua hatari zaidi kwani madktari walliwaambia wazazi wa Bradley kua mtoto wao ana miezi 2 tuu ya kuishi kutokana na kua kansa hiyo imeshasambaa sana katika mwili wa Bradley ni taarifa mbaya kwa mtu yoyote ila hasa kwa mzazi kusikia mtoto wao ana mwezi wa kuishi,baada ya kumuweka wazi mtoto wao kuhusu hilo mtoto wao aliamua kutumia siku zake za mwisho katika soka kwani ni shabiki mkubwa sana wa klabu ya Sunderland, amekua akikiongoza kikosi cha Sunderland kuingia katika mechi na amekua mascot wa Sunderland kwa muda mrefu, katika mechi ya mwisho Sunderland alipata heshima kubwa kwani aliweza kupiga penati iliyompita kipa wa Chelsea Asmir Begovic na kutimiza moja ya ndoto yake kubwa ya kuifungia goli timu yake aipendayo klaba ya kupiga penati hiyo mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa alimfuata Bradley na kumpa mbinu za kupiga mkwaju wa penati ili kumfunga Begovic na sasa goli lake limeingia katika magoli yatakayo shindanishwa kupata goli bora la mwezi katika ligi ya Uingereza, kwa sasa maisha ya Bradley ni tofauti kabisa na maisha anayotakiwa kuishi mtoto wa miaka mitano akianza kwa kutumia muda mwingi hospital kupata matibabu ya kansa ambayo hata watu wazima hulalamika kwa ucungu mkubwa kua ni matibabu yanayotesa ila zaidi ni kwamba Bradley anaishi akijua kwamba ana mwezi au miezi miwili ya kuishi ila kwa ujasiri ameonyeshwa kutotishika na hilo kwania amekua na furaha wakati wote. Mungu ana mipango yake kuyaruhusu yote haya yamtokee mtoto kama Bradley aliyepaswa kufurahia maisha yake kucheza pamoja na watoto wenzake hivyo kwa pamoja tunamtakia Bradley kila la heri mwenyezi Mungu amsimame naye kwa yote anayopitia.
Tags: #BradleyLowey
, Bradley Lowery
, Chelsea
, Neuroblastoma
, Sunderland
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






No comments:
Post a Comment