Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaFabregasLong unbeaten run

Chelsea wafunga mwaka kwa kishindo,Cahil,Willian na Diego Costa wacheka na nyavu Fabregas athibitisha yeye bado mkali.


Chelsea jana waliwapa mashabiki wao burudani ya aina yake baada ya kumaliza mwaka 2016 kwa kishindo kikubwa,katika mechi ya vuta ni kuvute funga nikufunge Chelsea walihakikisha wanajituma kwa kila namna kumaliza mwaka kwa kishindo Goli ya kwanza la Chelsea lilifungwa na Gary Cahill kabla ya Stoke kusawazisha Willian akaiweka Chelsea mbele tena ila Stoke wakasawazisha tena dakika za 69 Willian akaiongezea Chelsea goli la 3 na baadae diego Costa akaja kukamilisha kwa kufunga goli la nne na kufanya matokeo kua 4-2. kwa ushindi huo Chelsea waliifikia rekodi ya Arsenal ya kucheza mechi 13 bila kupoteza wala kudroo na kama wakishinda mechi ijayo basi watakua wamefikisha mechi 14 bila kufungwa na wataweka rekodi yao binafsi.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib