Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaCrystal palaceUchambuzi wa Crystal palace Vs Chelsea

Crystal Palace Vs Chelsea: Majeruhi,Vikosi vinavyotegemewa kuanza na mienendo ya timu zote mbili kwenye ligi.



Kuelekea mechi ya kesho ningependa kuwaletea ripoti fupi kuhusu mechi ya kesho nikiziangazia timu zote mbili Crystal Palace na Chelsea.

Crystal Palace wanatazimiwa kua bila Mathieu Flamin aliyepata majeraha katika mechi dhidi ya Manchester United, ila Jason Puncheon anategemewa kuwepo katika wachezaji ambao Alan Pardew anaweza kuawatumia katika safu ya kiungo baada ya mchezaji huyo kumaliza adhabu yake ya kutocheza mechi moja

Hiki ni kikosi kinachotazamiwa kuanza: Hennessey, Speroni, Ward, Dann, Delaney, Kelly, Fryers, Lee, Ledley, Phillips, Winter, Husin, McArthur, Townsend, Zaha, Cabaye, Mutch, Puncheon, Benteke, Campbell.

Chelsea wao watakua wakifurahia kurudi kwa mkali wao Eden Hazard aliyekua na majeraha ya kisigino,Hazard alishindwa kucheza mechi dhidi ya Sunderland ambapo Chelsea walifanikiw kuibuka kwa ushindi wa goli moja kwa bila. Mkongwe John Terry ataendelea kua nje ya uwanja kutokana na majeruhi pia ila inatazamiwa Zouma anaweza akacheza mechi yake ya kwanza msimu huu baada ya kuwa katika bemchi mechi iliyopita.

Hiki ni kikosi kinachotazamiwa kuanza: Courtois, Begovic, Alonso, Fabregas, Zouma, Kante, Oscar, Hazard, Pedro, Loftus-Cheek, Moses, Costa, Matic, Willian, Batshuayi, Cahill, Azpilicueta, Chalobah, Luiz, Eduardo, Aina, Solanke.
 
Mechi tano za mwisho za Crystal Palace:LDWLL
Mechi tano za mwisho za Chelsea: WWWWW

Katika mechi walizowahi kukutana Crystal Palace ameshinda mechi 6 ametoa droo 14 huku Chelsea akifanikiwa kushinda mechi 18. Mechi itachezwa saa 12:30 mchana kwa majira ya Uingereza inategemewa kua saa 2:30 mchana kwa majira ya Afrika mashariki na itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Sky Sport 1

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib