Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaManchester unitedMikel ObiMikel to Tianjin TEDA

John Mikel Obi miaka 10,makocha 10 mechi 372 makombe 8. Usajili wake uligubikwa na utata kwa kusajiliwa na Man U na Chelsea kwa wakati moja.






John Mikel Obi alifika Chelsea akiwa na miaka 19 tuu huku usajili wake ukigubikwa na utata kwani Manchester United wakimsajili na kumtambulisha rasmi lakini baadaye Chelsea wakapinga wakisema kua wao ndio walikua wa kwanza kumsajili na kumsainisha mkataba kutokana na mzozo huo Manchester United waligoma kumuachilia mpaka walipwe paundi milioni 12 wakati wao walikua wamemsajili kwa paundi milioni nne tuu. Hivyo Chelsea wakaamua kuwalipa Manchester United kiasi hicho cha pesa na kumchukua Mikel Obi,baada ya Mikel kutua Chelsea alikua na mtihani mkubwa kuonyesha uwezo wake kwani timu mbili kubwa Uingereza zilikua zikiwania saini yake hata hivyo haukua msimu mbaya kwake kwani alifanikiwa kucheza jumla ya mechi 22 akiwa ameisaidia Chelsea kushinda kombe la FA na Carling Cup pamoja na kuchaguliwa kua mchezaji bora kijana katika sherehe za mwisho wa mwaka,baada ya hapo kwa mikel ilikua ni mafanikio kwani aliichezea Chelsea mechi 372 chini ya mameneja 10 na wote hao hamna hata moja aliyefikiria kumuuza,kocha Guus Hiddink alionekana ni shabiki mkubwa wa Mikel katika awamu zote mbili alizoifundisha Chelsea. Katika vyote ambavyo Mikel ameifanyia Chelsea mashabiki wa Chelsea watakumbuka sana kiwango chake katika msimu wa mwaka 2012 hasa katika kombe la UEFA kwani alicheza dakika zote 90 kuanzia mechi za  robo fainali mpaka fainali kwani wiki moja kabla ya fainali ya UEFA alikua amecheza dakika 90 pia kwenye fainali ya FA dhidi ya Liverpool na kuisaidia Chelsea kuchukua kombe hilo. Mashabiki wengi wa Chelsea wanampenda Mikel kwa ukarimu upole na tabia ya kua sawa kwa kila mtu anayekutana nae kitu kilichompatia umaarufu mkubwa kwa mashabiki wa Chelsea.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib