Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Branislav IvanovicBrentfordChelseaChelsea wonderkidsFabregasIvanovicWillianwonderkids

Uchambuzi wa mechi kati ya Chelsea Vs Brentford. Chelsea 4-0 Brentford

Chelsea waliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza klabu ya Brentford magoli manne kwa bila yafuatayo ni baadhi ya mambo tuliyoweza kuyachambua kutoka kwenye mechi ya jana.

1.Conte kubadilisha wachezaji 9 kikosi cha kwanza.
Kocha Antonio Conte jana alifanya mabadiliko katika kikosi chake huku akiwaanzisha sana vijana wadogo kama akina Chalobaha,Ruben,Ake,Zouma na Batshuayi pia alifanya mabadiliko kwenye nafasi ya mlinga mlango ambapo jana Begovic akilinda lango na Eduado akiwa benchi kama kipa wa akiba kwa maana hiyo inaonekana Chelsea wana kikosi kipana kwani wana wachezaji wengi ambao wanafanya vizuri pindi wanapopewa nafasi.

2..Ivanovic awaaga mashabiki wa Chelsea.
Beki huyo anategemewa kuondoka klabu ya Chelsea wiki hii baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa muongo moja(Miaka 10) na kocha Antonio Conte aliamua kumpa heshima yake kwa kumpa nafasi kipindi cha pili ambayo beki huyo aliitumia vizuri na kuweza kufunga goli zuri ambalo ni kama kwa heri kwa mashabiki wa Chelsea.

3.Fabregas ammkumbusha Conte kua yeye bado ni muhimu kwenye timu.
Fabregas bado hajapata nafasi ya kuanza kwenye mechi ya ligi kuu tangu mwaka 2017 uanze na amekua akihusishwa kuhamia nchini Italy huku klabu kama Juventus na AC Milana zikiweka bayana kua zina mhitaji ila kiungo huyo jana alimuonyesha Conte yeye bado ni muhimu katika kikosi cha Chelsea kwani alimiliki kiungo vizuri na kuweza kutengeneza mipira mizuri kuelekea kwa mawinga na washambuliaji na kua mwimba kwa timu ya Brentford na kuchaguliwa kua mchezaji bora wa mechi.
4.Kenedy na Ake warudi darajani.
Kijana wa kibrazili aliyejaliwa kipaji cha kucheza namba nyingi tofauti kama beki wa kushoto,winga wa kulia na kushoto na hata mshambuliaji jana alicheza mechi yake ya kwanza china ya Antonio Conte akiingia kama mchezaji wa akiba,watu wengi wanatumaini mchezaji huyo atafanya vizuri kwa kua Conte anapenda kuwapa nafasi vijana.Pia beki wa kushoto mwingine Nathan Ake alicheza mechi yake ya kwanzachini ya Conte baada ya kurudishwa katika timu aliyokua akiichezea kwa mkopo.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib