Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Arjen RobbenChelseaDrogbaEden HazardManchester unitedMikel ObiPedroVictor Lindelof

Wachezaji watano waliokua wanasajiliwa na Manchester United lakini Chelsea wakawawahi dakika za mwisho.


Mashabiki wa Manchester united walikua wamejihakikishia kumsajili beki wa Benefica Victor Lindelof ila habari mbaya kwao ni kwamba Chelsea nao wamesema wanamtaka beki huyo ambaye anategemewa kuuzwa wakati wa majira ya joto baada ya mismu kumalizika.  Na hii ni listi kamili ya wachezaji ambao Chelsea iliwasajili wakiwa wameshafanya mazungumzo na Manchester United.

  1. Eden Hazard.
Kabla ya kujiunga na Chelsea akitokea klabu ya Lille Eden Hazard alikutana na kocha wa Manchester United kipindi hicho Sir Alex Fergueson ambaye alikua akifanya kila jitihada kumsajili winga huyo wa Ubelgiji kwenda Old Trafford. Ndipo mmiliki wa Chelsea tajiri Roman Abramovich alipoamua kujitosa yeye mwenyewe kumsajili Eden Hazard, Hazard alisimulia kua alikutana na Abramovich na mazungumzo yalikua mafupi sana ila Abramovich alimuambia kua timu zote Man U na Chelsea wanamhitaji ila Chelsea wana project kubwa siku za usoni hivyo ilimvutia Eden Hazard kujiunga na Chelsea.
Eden Hazard akitambulishwa baada ya kusajiliwa na Chelsea.
 2. Arjen Robben

Arjen Robben alikua ni kama ameshakua mchezaji wa Manchester United kwani kabla ya kusajiliwa alitembezwa yeye na baba yake kuuona uwanja wa Old Trafford pamoja na uwanja wa kufanyia mazoezi wa Carrington anasema alivyokutana na Sir Alex alikua tayari kusain mkataba na Manchester ila alishauriwa na aliyekuwa kocha wa Chelsea kipindi hicho Claudio Ranier kuachana na Man United na kujiunga nao alisema sijutii kutokuichagua Manchester united kwani kwenye mpira mambo yanabadilika haraka.
Arjen Robben akishangilia goli.
3. Pedro
Usajili wa Pedro kutoka Barcelona kwenda Chelsea uliwafanya Manchester United kupoteza imani na makamu wa rais wao anayesimamia masuala ya usajili wa wachezaji Mr. Edward Woodward kwani alipanda ndege kwenda nchini Hispania kukutana na Pedro pamoja na klanu yake ya Barcelona  hivyo kuwafanya mashabiki kuamini kua Pedro atatua Old Trafford siku za usoni ila winga huyo hakutokea mwishoni wakasikia kua amesajiliwa na klabu ya Chelsea

4.Didier Drogba

Drogba aligeuka kua shubiri kwa timu za ligi kuu kitu kilichomfanya Sir Alex Kujutia kumkosa na aliweka wazi kwenye kitabu alichokiandika kua yeye mwenyewe alisafiri mpaka jiji la Marseille nchini Ufaransa kwenda kumshuhudia Didier Drogba akicheza baada ya kuridhika nae maongezi yalianza ambapo klabu ya Marseille walikua wakitaka wapewe kiasi cha paundi milioni 25 wakati Man U wakisua sua klabu ya Chelsea walikuja na nguvu zote wakakamilisha usajili na kumtangaza na kuwaacha United wakishangaa kilichotokea kwani baada ya hapo ilikua ni historia Drogba alifanya vizuri na kua moja ama mchezaji bora kabisa kutokea bara la Afrika

5.John Mikel Obi
John Mikel ndiye mchezaji aliyeleta utata zaidi sio kukaribia kusajiliwa tuu bali alikua ameshasajiliwa na Manchester United,Chelsea wakakata rufaa wakisema wao walishafanya nae makubaliano mchezaji huyo ila hapo Manchester United walikua wakali wakata kulipwa pesa zao ili wamuachie Mikel Chelsea hakua na budi kwani aliamua kuwalipa pesa na kumchukua Mikel Obi.

Mkataba aliosaini Mikel Obi na Klabu ya Manchester United.


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib