Climb the mountains
Antonio ConteAntonio Conte new ContractChelsealondonmkataba mpya
Antonio Conte afikia makubaliano ya kuboresha na kuongeza mkataba.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte amefikia makubaliano na klabu yake ya Chelsea kuhusu kuongeza mkataba wake baada ya kuwafurahisha mabosi na mashabiki wa Chelsea kwa kuifanya timu yao kua ya kuogopwa kama zamani. Conte kupewa mkataba mpya ilikua ni kitendo cha wakati tuu kwani tangu ajiunge na klabu ya Chelsea akichukua nafasi ya Guus Hiddink ambaye nae alichaguliwa kua kocha wa muda baada ya Jose Mourinho kufukuzwa. Tangu Conte atue Chelsea amepoteza michezo mitatu tuu huku akiifikia rekodi ya Arsenal ya kushinda mechi 13 mfululizo. Taarifa za kuaminika kutoka vyanzo vya habri ndani ya klabu ya Chelsea vinasema kocha huyo amefikia makubaliano ya kuongeza mkataba utakaofika kikomo mwaka 2020 baada ya ule wa kwanza uliokua unaisha mwaka 2019.Chelsea kumpa Conte mkataba mpya akiwa hajamaliza hata mwaka moja klabuni ni hapo ni ishara tosha kua matajiri hao wa London wamefurahishwa na kuridhishwa na kiwango cha kocha huyo pamoja na matokeo chanya aliyoyaleta katika kikosi chake ndani ya muda mfupi.
Tags: Antonio Conte
, Antonio Conte new Contract
, Chelsea
, london
, mkataba mpya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment