Mwezi moja uliopita kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourihno aliirushia dongo klabu yake akisema kua wanacheza mpira wa kujilinda na watashinda ligi kwa mbinu zisizofaa, pia akasema kocha Antonio Conte anatumiambinu ambazo yeye alizitumia maika yake yote aliyokua Chelsea na anashangaa kwanini yeye hakusifiwa mbinu zake zilivyokua zinafanikiwa kama anvyosifiwa Conte.Leo nimeona nichambue vitu vichache tuu kati ya Mourihno alivyokua Chelsea na sasa Conte akiwa kama kocha nakuomba uwe nami na ninaamini unaweza kubaliana nanyo au pia unaweza kua mtazamo tofauti kidogo au sana ila kwa mashabiki wa soka kua na mtazamo tofauti ni kitu cha kawaida na pia ndio kitu inachofanya tuipende soka zaidi kwani hapo ndipo unapooanza ubishani wa soka, ubishani unaoweza kumfanya shabiki wa soka akapitiliza hata muda wa kula.
Conte ameifanya Chelsea ipendwe tena.
Nakumbuka wakati Jose Mourinho alipokua akiifundisha Chelsea alikua akikosolewa sana kwa mbinu zake za kupaki basi, kwa alikua akipata goli moja tuu katika baadhi ya mechi anabadili mfumo na kupaki basi mbinu zilizokua zinawakera sana makocha,wachezaji na mashabiki wa timu pinzani japo kwa Chelsea walikua wanapata walichokua wanakihitaji namaanisha ushindi, mbinu za kupaki basi zilifanya timu nyingi na mashabiki wao wachukie kucheza na Chelsea wakisema tunacheza mpira wa miaka ya 60 mpira usiovutia na walisema tunashinda mechi tusizostahili nakumbuka mwaka juzi ilikua ni timu ya kwanza katika timu zinazochukiwa zaidi duniani wengi wakisema inachukiwa sababu ya mbinu zake mbaya za kujilinda tuu na kuharibu ladha ya mpira. Tangu kocha Antonio Conte achukue mikoba imekua historia kwani sasa Chelsea inacheza mpira wa kuvutia na pia wachezaji wake wamekua kwenye kiwango kizuri.
2.Wachezaji chipukizi wanapewa nafasi.
Japo ndo kwanza ni msimu wake wa kwanza ila Antonio Conte ameonyesha kitu cha tofauti na Jose kwani pia ameonyesha kuwaamini wachezaji chipukizi zaid ya Mourihno, Jose tutamkumbuka kwa kumpa nafasi Kurt Zouma ambaye alikua anaelekea kua beki bora kabisa kabla ya kupata majeruhi yaliyomuweka nje ya uwanja kwa mwaka moja pia Jose aliwapa nafasi nyota wengi wadogo awamuu yake ya kwanza Chelsea japo alikua anawapa kwenye mechi ambazo Chelsea haikua na cha kupoteza kwani mechi walizokua wanacheza Chelsea alikua ameshatangazwa bingwa. Conte amewapa nafasi wachezaji wengi chipukizi tukianzia,Nathaniel Chalobah,Ruben Loftu-Cheek,Ola Aina, tofauti ya Conte na Jose ni kua Conte amewapa nafasi hata kwenye mechi za ushindani tena mwanzo wa ligi kama mechi dhidi ya Leicester City ambayo aliwaanzisha Nathaniel Chaloba na Ruben kwenye nafasi ya kiungo
3.Wachezaji wanaotolewa kwa mkopo wanaanza kutumika kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea.
Pamoja na kua anawapa nafasi vijana wadogo pia wachezaji wanaotolewa kwa mkopo ili wakaimarishe viwango vyao kabla ya kuaminiwa na kupewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea wameaanza kupata matumaini baada ya Nathan Ake ambaye alitolewa kwa mkopo kufanya vizuri katika timu ya Bournmouth na kuitwa kukitumikia kikosi cha Chelsea. Pia hivi juzi kocha Antonio Conte alikua akimuaangalia beki Tomas Kalas kwenye mechi kati ya Tottenham na Fulham kijana ambaye alikua kwenye kiwango cha juu sana miaka michache iliyopita lakini alishindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha Chelsea hivyo ikasababisha kiwango chake kuporomoka, pia Conte amegusia uwezekano wa wachezaji kama Andreas Christensen kurudi darajani msimu ujao.
No comments:
Post a Comment