Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Carlo CudiciniConteFA CupFA Cup 2016/17 QUARTER FINALFulhamLucas PiazonRyan SessegnonTomas Kalastottenham

Antonio Conte alikua akiaangalia mechi ya Fulham Vs Tottenham je ni nani alikua anamfuatilia?Vijana wa Chelsea walio kwa mkopo au Ryan Sessegnon?




Baada ya ushindi dhidi ya Wolves juzi kocha Antonio Conte angeweza kupumzika nyumbani siku ya jana au kwenda nyumbani kwake Italia mara moja au kutoka out na kikosi chake kwenda kwenye hoteli za hadhi ya juu kupiga chakula cha jioni ila muitaliano huyo aliweka kazi yake mbele na kuamua kwenda kuangalia mechi kati ya Fulham na Tottenham huku akiongozana na Carlo Cudicini kipa wa zamani wa Chelsea kitu ambacho hakikutarajiwa kabisa na watu wengi. Swali kubwa mpaka sasa ni mchezaji gani alienda kumuangalia? Jibu la haraka linaweza kua alienda kuangalia maendeleo ya wachezaji wa Chelsea waliotolewa kwa mkopo kwenye klabu hiyo na pengine aliyemvuta kwenda kwenye mechi hiyo anaweza kua mlinzi wa kati Tomas Kalas ambaye alianza kwenye mechi ya jana. Mlinzi huyo wa kati mwenye miaka 23 aliwahi kutajwa kama moja ya wachezaji watakao kuja kufanya vizuri sana siku za usoni na takumbukwa kwenye mechi kati ya Chelsea na Liverpool mwaka 2015 kwani aliweza kumdhibiti aliyekua mpachika mabao wa Liverpool kipindi hicho Luis Suarez,pia anatajwa Lucas Piazon Mbrazili mwenye miaka 23 naye ambaye aliwahi kutajwa kama Ricardo Kaka mpya ila alishindwa kung'aa na hata kwenye mechi ya jana aliachwa benchi. Ryan Sessegnon anatajwa kua mchezaji mwingine aliyemfanya kocha Antonio Conte akaangalie mechi hiyo kwani tetesi zinasema klabu ya Chelsea ni moja ya klabu kubwa zinazo ifukuzia saini ya kinda huyo mwenye miaka 16 tuu anayecheza nafasi ya beki wa kushoto
Lucas Piazon





Tomas Kalas anatajwa kua ndo mchezaji aliyekua akiaangaliwa kwa ukaribu zaidi na Conte




Ryan Sessegnon amekua akifukuziwa na klabu kubwa barani Ulaya na Chelsea ikiwa mojawapo

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib