Climb the mountains
Chelsea vs Manchester UnitedJose MourihnoJose Mourihno Mind Games
Jose Mourinho: Tayari Chelsea ni mabingwa wa ligi kuu. Je unahisi sifa hizi ni za kweli au mind games za Mourinho?
Klabu ya Manchester United imepangwa kucheza na klabu ya Chelsea katika mechi ya kombe la FA hatua ya robo fainali itakayochezwa katika dimba la Stamford Bridge(Darajani) na kocha wa Manchester United Jose Mourinho alisema kua tayari klabu ya Chelsea ni mabingwa kwenye ligi hivyo inawapatia mwanya wa kuelekeza nguvu zote kwenye FA kwa kua hawana cha kupoteza kwenye ligi tofauti na Manchester United ambao bado wanapigana kuhakikisha wanaingia nne bora na kufanya vizuri kombe la Europa. Katika maongezi hayo Jose alionekena akiisifia sana Chelsea na kuwahakikishia kua wao ni bora kuliko timu yake na wana ratiba rahisi kitu ambacho watu walitafsiri kama ameaanza kucheza mind games na Chelsea ili wawe na uhakika wa kuifunga Manchester United alafu yeye aje na mbinu itakayowashangaza kama ilivyozoeleka .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment