Climb the mountains
Antonio ConteChelseaKurt Zouma
Kurt Zouma aongelea mipango yake kama hatapata namba ya kudumu kwenye klabu ya Chelsea
Beki chipukizi wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa amesema kua atafikiria hatma yake Chelsea mwisho wa msimu au baada ya msimu ujao kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi January. Zouma alisema anafurahi anapata namba kwenye mechi za kombe la ligi na baadhi ya mechi za ligi kuu ila kwa umri wake yeye anahitaji kucheza mechi nyingi kwani bado ni chipukizi na yupo kwenye kiwango kizuri kiasi licha ya kurudi kutoka kwenye majeraha hivyo hatakua tayari kukipoteza kwa kukaa benchi. Zouma pia alikiri kua anatanguliza timu mbele kuliko maslahi yake binafsi na anamshukuru sana kocha Antonio Conte kwani alimpa faraja akiwa ameumia na hata alipopona alimuamini na kumpa nafasi ya kuanza kucheza tena kwenye kikosi cha kwanza.
Tags: Antonio Conte
, Chelsea
, Kurt Zouma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment