Climb the mountains
Arsene WengerChelseaLeicester CityN'golo KanteRyan Giggs
Ryan Giggs anatamani Manchester United wangewashinda Chelsea kwenye usajili wa N'golo Kante.
Mkongwe wa klabu ya Manchester United ambaye pia amekua shabiki mkubwa wa N'golo Kante tangu akiwa Leicester ameweka wazi kua anatamani sana kalbu yake ya zamani Manchester United wangewapiku Chelsea kwenye kumsajili kiungo Kante,Giggs alisema "Kiukweli msimu uliopita nilipenda sana klabu yangu ingemsajili Kante kwani alikua akiuzwa kwa ada ndogo ya paundi milioni 29, Kante ni mchezaji anayewinda mpira ni mchezaji mwepesi sana kulinda sehemu zilizo wazi, nimewahi kucheza na mchezaji wa aina ya Kante kipindi bado nacheza mpira ni kitu cha kukupa hofu sana kwani ni ngumu kumkabili. Giggs sio mtu pekee aliyekiri kumpenda Kante kwani kocha wa Arsenal pia Arsene Wenger alikiri kua alijaribu kumsajili Kante mara mbili mara ya kwanza alizidiwa kete na Leicester na mara ya pili alizidiwa kete na Chelsea.
Tags: Arsene Wenger
, Chelsea
, Leicester City
, N'golo Kante
, Ryan Giggs
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment