Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Cesc FabregasChelseaFabregas to Real MadridMadridzidane

Wakati akiendelea kukosa namba ya kudumu Chelsea,tetesi zinasema Real Madrid wanamtaka Cesc Fabregas


Kiungo Fabregas amepata wakati mgumu msimu huu kupata namba kwenye kikosi Chelsea kwani bosi Antonio Conte amekua akimtumia zaidi Kante na Nemanja Matic katika safu ya kiungo na amekua akimtumia Pedro na Willian kama viungo wachezeshaji na muda mwingine mawinga kitu ambacho kimemnyima Fabregas kupata nafasi. Klabu mbali mbali zilionyesha nia ya kumsajili pamoja na kua klabu yake ya Chelsea ilikua tayari kumuuza ila yeye aliweka bayana kua hafikirii kuondoka klabuni hapo na atabakia kupambana ili kuirudisha nafasi yake amekua akipewa muda mchache au kuanza mechi za kombe la Capital One na mechi zote alizopewa nafasi amekua akifanya vizuri ikiwa pamoja na kufunga magoli kutengeneza magoli hata kua mchezaji bora wa mechi, ila kwa sasa taarifa ni tofauti na awali wanaomtaka kwa sasa sio klabu ndogo kama za awali ilivyokua ila ni miamba ya soka duniani maaduai zake tangu utotoni yani Real Madrid wanasema kwenye mpira hakuna adui wa kudumu na msemo huo unaweza kutimia kama kiungo huyo atajiunga na mahasimu wake wa zamani kama alivyofanya wakati akijiunga na klabu ya Chelsea ambao ni mahasimu wa klabu yake ya zamani ya Arsenal ila maisha hayakukwama yalisonga mbele. Kuna uwezekano mkubwa sana wa Fabregas kuondoka mwisho wa msimu kwani Chelsea wanafikiria kumuuza ili kupata pesa zaidi za usajili ila klabu atakayojiunga nayo ni maamuzi yake yeye mwenyewe

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib