Climb the mountains
Best in WorldCristiano RonaldoEden HazardHazard BrothersLionel MessiThorgan Hazard
Thorgan Hazard: Kaka yangu ni mchezaji watatu kwa ubora duniani.
Mdogo wake Eden Hazard ambaye pia ameshawahi kukipiga ndani ya klabu ya Chelsea alifunguka kuhusu kiwango cha kaka yake ambaye yupo kwenye fomu nzuri msimu huu na kusema anavyohisi kiwango cha kaka yake kinampa nafasi gani pamoja na wachezaji wengine duniani. Thorgan Hazard alisema"Watu wengi wanasema Eden Hazard akiendelea kucheza vizuri atakua moja ya mchezaji bora duniani kwa sasa tuna Cristiano Ronaldo pamoja na Lionel Messi kama wachezaji bora kabisa kupata kutokea na pengine kaka yangu itamlazimu kusubiri mpaka wawili hao watakapo staafu au kuzeeka kabisa ili kuwapiku ila kwangu mimi Eden Hazard ni mchezaji bora duniani nadhani akitoka Messi na Ronaldo basi anafuata Eden Hazard ningependa siku moja anakua watatu kwenye orodha ya Ballon d'Or akiwafuata Messi na Ronaldo na siku moja aje kuchukua kabisa" Eden Hazard alijaribu kuisogelea tuzo ya Ballon d'Or mwaka 2015 ambapo aliishika nafasi ya nane.
Tags: Best in World
, Cristiano Ronaldo
, Eden Hazard
, Hazard Brothers
, Lionel Messi
, Thorgan Hazard
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment