Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

AgueroChelseaChinese Super LeagueInter MilanManchester CityParis Saint Germainreal madrid

Wakati Pep Guadiola akimuweka benchi Sergio Aguero kwa mechi ya pili mfululizo na kuibua sintofahamu kuhusu hatma ya kiungo huyo hizi ni timu sita anazoweza kujiunga nazo msimu ujao.


Hakuna shabiki wa soka asiyelifahamu jina la Sergio Aguero na hakuna mfuatiliaji wa mpira wa ulaya asiyefahamu uwezo wa Aguero uwanjani jinsi anavyojituma na alivyo shapu kufunga magoli unaweza sema ni mtu aliyezoea kutikisa nyavu lakini mambo ni tofauti kwake msimu huu si kwa sababu ameshuka kiwango hapana ila ni mabadiliko ya mfumo ndani ya Manchester City,kocha Guadiola alionyesha kutopendezwa na Aguero tangu wakati anatua City ila kwa sasa amezidisha hasa baada ya mshambuliaji wao Gabriel Jesus kujiunga nao na kuaanza kucheza Guadiola alimuweka benchi Aguero kwa mechi mbili mfululizo na katika mechi hizo zote Gabriel Jesus aliyepewa nafasi ya Aguero alifanikiwa kufunga magoli,kuna uhakika mkubwa kua Aguero ataondoka City mwisho wa msimu huu je ataenda timu gani? nakuchambulia timu 6 ambazo kwa hakika lazima tutamuona Aguero huko iwapo ataondoka Manchester City.



    Chelsea                                                                                                                                          Antonio Conte ameifanya Chelsea kua tishio kama zamani na wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 9 na timu inayowafuatia ila kwa kashikashi aliyowapa Diego Costa hivi karibuni huenda Chelsea wakamfikiria Aguero kama mbadala rasmi wa Diego Costa na kama ataendelea kuachwa benchi kwenye mechi za Manchester City basi kitu hicho kitawachochea Chelsea kumsajili.  
      Real Madrid                                                                                                                                  Mfaransa Karim Benzema ameashiria kua ataondoka Madrid mwisho wa msimu huu Zinadine Zidane anaweza kumuuza Benzema ili kupata pesa atakazo ongezea kumsajili Aguero,pia Aguero amekua akihusishwa kujiunga na klabu ya Manchester City mara kadhaa huenda sasa akamua Madrid iwe timu yake mpya.
        Paris Saint-Germain                                                                                                                     Inasemekana matajiri kutoka jiji la Paris wanafuatilia hali ya Aguero Manchester City kwa ukaribu sana,japo PSG wamemuweka Alexis Sanchez kama mchezaji wa kwanza wanayemuhitaji msimu ujao ila Aguero kwa sasa anaangaliwa kama mbadala wenye uhakika na matajiri wa klabu hiyo kutoka Qatar wanao uwezo wa kifedha kumshawishi Aguero kujiunga nao.
          Inter Milan                                                                                                                                     Inter Milan wanajiandaa kufanya usajili utakao washtukiza wengi na miezi kadhaa iliyopita waliwahi kuwauliza Manchester City ikiwa wanaweza kuwauzia Aguero lakini City walikataa ila kwa hali ilivyo sasa Inter Milan wameshawishika kumpa Aguero msaada wa kuanza upya maisha yake ya soka kwani na klabu hiyo kwa sasa iko kwenye project ya kujenga upya klabu yao hivyo kumsajili Aguero itakua moja ya kuafanikisha lngo kubwa la klabu la kusajili wachezaji nyota.
            Chinese Super League                                                                                                                   Ligi kuu ya China imekua tishio miaka ya karibuni kwa kuwasajili wachezaji wenye majina makubwa kutoka ulaya na wamekua wakiwasajili kwa pesa kubwa sana pamoja na kuwalipa mishahara ya kufuru hata kuwazidi Cristiano Ronaldo na Messi wachezaji bora kabisa duniani kwa muda mrefu. Hivyo haitakua ajabu kama kuna timu kutoka ligi kuu ya China itaamua kumsajili nyota huyo.
              Kubakia Manchester City                                                                                                             Pamoja na yote yanayoendelea klabu yake ya Manchester City wamesema kua Aguero ataendelea kubaki Manchester City msimu ujao na wanategemea nyota huyo atapigania nafasi yake dhini ya mshambuliaji chipukizi Gabriel Jesus.

                No comments:

                Post a Comment

                Bottom Ad [Post Page]

                | Designed by Colorlib