Climb the mountains
BarcelonaConteConte amkataa NeymarNeymar
Antonio Conte azuia usajili wa Neymar licha ya Abramovich kukubali kuwalipa Barcelona £155 milioni.
Katika taarifaa zilizowashangaza mashabiki wengi wa soka wiki hii moja wapo ni ya kocha wa Chelsea Antonio Conte kuzuia Chelsea wasimsajili nyota wa Barcelona kwa dau la £155 milioni ambalo lingevunja kabisa rekodi ya dunia. Inaripotiwa mmiliki wa Chelsea bilionea Roman Abramovich alishamaliza mazungumzo na klabu ya Barcelona ambapo alikubali kuwalipa pesa wanayotaka ila katika hali ya kushangaza kocha wake akazuia usajili huo, Abramovich anafanya kila jitihada kuhakikisha anambakisha Antonio Conte Chelsea baada ya klabu ya Inter Milan kuweka wazi inamtaka kocha huyo na wapo tayari kumpa kiasi chochote cha pesa atachohitaji kumsajili wachezaji wa chaguo lake. Inasemekana Conte anataka kukipunguza kikosi chake kwanza kabla hajaanza kusajili na haamini kama Neymar anaendana na aina ya uchezaji anaoutaka yeye pia Conte aliwaambia viongozi wa klabu kua anataka kua muamuzi mkuu wa masuala ya usajili katika klabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment