Habari zinasema klabu ya Barcelona inajiandaa kufanya mageuzi makubwa kwenye kikosi chao msimu ujao baada ya kua na matokeo mabaya katika mechi nyingi msimu huu. Siku ya jumatatu wakati Chelsea ikimenyana na klabu ya West Ham mascout wa Barcelona walikua moja ya watazamaji wa mechi hiyo akiwemo Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Mr. Robert Fernandez. Wakati mashabiki wengine tukiwaza hasa kuhusu kushinda mechi hiyo mascout hao walikua na kazi binafsi ya kuwaangalia nyota watatu wa Chelsea ambao ni Cesar Azpilcueta, Nemanja Matic na Marcos Alonso. Azpilicueta na Alonso wote hawa waling’aa katika mechi hiyo ambayo Chelsea ilishinda goli mbili kwa moja huku Nemanja Matic yeye akiingia dakika 20 za mchezo. Barcelona wamekua wakihangaika sana kuimalisha safu yao ya ulinzi ambayo imekua na udhaifu hasa baada ya beki wao mkongwe Dani Alves kuondoka klabuni hapo hivyo walikua wakiwaangalia Alonso na Azpilicueta ili kuamua ni mchezaji gani wanahakikisha wanamsajili wakati wa dirisha la usajili pia walimuangalia beki wa Arsenal Hector Bellerin ambaye zamani alikua mchezaji wao kabla hawajamuuza kwenda Arsenal.
Climb the mountains
BarcelonaBarcelona scout chelsea playersCeser AzpilicuetaChelseaMarcos AlonsoNemanja matic
Barcelona iliwatuma mascout na Mkurugenzi wake kuwaangalia nyota watatu wa Chelsea katika mechi dhidi ya West Ham.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





No comments:
Post a Comment