Klabu ya Real Madrid wamekua wakimfukuzia Eden Hazard kwa miaka kadhaa na wamekua na matumaini makubwa ya kumpata mchezaji huyo kwa kua Eden Hazard ni shabiki mkubwa sana wa kocha wa Real Madrid Zinadine Zidane,miaka ya nyuma Hazard alikaririwa akisema angependa kucheza chini ya kocha Zidane siku moja. Lakini habari kutoka Evening Standard zinasema kua winga huyo hatailazimisha klabu yake ya Chelsea imuuze hata kama Real Madrid wakituma ofa ya kumsajili kwani mwanzo wa msimu huu alikaririwa akisema “Nitaondoka baada ya kushinda makombe.Unavyoondoka lazima uondoke ukiwa wa hadhi ya juu ukiwa umewaachia mashabiki kitu kizuri na sahihi cha kukumbuka” Hata hivyo kwa sasa gazeti hilo limesema Eden Hazard na familia yake wanaishi vizuri Uingereza n ahata kama Chelsea watashinda ligi msimu huu hana mpango wa kuondoka.
Eden Hazard amefunga magoli 11 msimu huu baada ya kocha Antonio Conte kumpa jukumu kubwa la kati katika mfumo wake wa 4-3-3 na sasa anajiandaa na wachezaji wenzake wa Chelsea na mechi ya FA dhidi ya Manchester United itakayochezwa jumatatu wakiwa na nia ya kufukuzia makombe mawili msimu huu



No comments:
Post a Comment