Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaChelsea to sell BatshuayiMitch BatshuayitottenhamWest Ham

Chelsea wako tayari kumuuza Batshuayi ikiwa ni mwaka moja tuu tangu wamsajili.


Klabu ya Chelsea wako tayari kumuuza mshambuliaji waliyemnunua kwa fedha nyingi Mitchy Batshuayi wakati wa dirisha kubwa la usajili baada ya kutoridhishwa na kiwango cha nyota huyo. Batshuayi aliyekua anatakwa na klabu ya West Ham na Tottenham alizikataa klabu hizo na kuamua kujiunga na klabu ya Chelsea ambapo ameshindwa kumshawishi kocha Antonio Conte kumpatia nafasi za mara kwa mara kwenye kikosi chake,mara ya mwisho Batshuayi kucheza alikua ni tarehe 12 mwezi wa 2 mechi kati ya Chelsea Vs Burnley ambapo aliingia dakika tatu za mwishoni. Japo mashabiki wengi wamekua wakimuomba kocha Antonio Conte asimuuze mchezaji huyo wakimtaka ampe muda zaidi au amtoe kwa mkopo kwani wanaamini nyota huyo anauwezo mkubwa na wamekua wakilinganisha hali yake na Victor Moses ambaye alionekana hana uwezo wa kuichezea Chelsea lakini ameweza kurudi katika kiwango chake na kufanya vizuri. Je unadhani Chelsea watakua sahihi kumuuza Batshuayi?

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib