Climb the mountains
Antonio ConteChelseaInter MilanInter Milan want ConteItaly
Chelsea wanaamini Antonio Conte atakataa ofa kutoka Inter Milan. Inter Milan wapo tayari kumlipa Antonio Conte paundi milioni 10 kwa mwaka.
Klabu ya Chelsea wanaamini kocha wao Antonio Conte ataikataa ofa nono kutoka klabu ya Italy Inter Milan ambapo wako tayari kumlipa paundi milioni 10 kwa mwaka na pia wamemuahidi pesa kubwa ya kufanyia usajili pindi atapokubali kujiunga nao. Conte ambaye kwa sasa anaishi pekee yake Uingereza huku familia yake ikiwa bado ipo nchini Italia lakini taarifa zinasema wanafanya taratibu za kuhamia London siku za usoni. Hata hivyo ikiwa Inter Milan watafanikiwa kumshawishi Conte bado watakua na kazi ya ziada kwani Antonio Conte amesaini mkataba mpya mwezi uliopita hivyo itawabidi kuwalipa Chelsea pesa nyingi kwani Chelsea wanamlipa paundi milioni 15 kwa mwaka na mkataba wake unakadiriwa kua na thamani ya paundi milioni 60 kitu ambacho hakitakua kibaya sana kwa Chelsea ikiwa Inter Milan watamnunua kocha huyo kutoka Chelsea.
Tags: Antonio Conte
, Chelsea
, Inter Milan
, Inter Milan want Conte
, Italy
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment