Climb the mountains
CheleaNew ContractNigeriaVictor MosesVictor Moses sign new contract
Victor Moses asaini mkataba mpya. Yawekwa wazi jinsi klabu ya West Ham walivyomkataa kwa kiwango kibovu na kumrudisha Chelsea.
Winga wa Chelsea na timu ya taifa ya Nigeria Victor Moses jana aliongeza mkataba wa miaka miwili katika mkataba wake wa awali na sasa kufanya mkataba wake kuisha mwaka 2021 baada ya mwaka 2019 pia mshahara anaolipwa nyota huyo umepanda kufikia paundi elfu 75 kwa wiki. Moses alikua moja ya wachezaji waliosahaulika Chelsea na hivyo kutolewa kwa mkopo mara kadhaa na mara ya mwisho alitolewa kwa mkpo katika klabu ya west Ham ambapo baadae Chelsea waliwaomba West Ham wamnunue mchezaji huyo awe wao moja kwa moja kitu ambacho West Ham walikataa kata kata wakidai hawajaridhiswa na kiwango cha winga huyo hivyo hawezi kupata nafasi katika kikosi chao. Baada ya kocha mpya Antonio Conte kuanza kuifundisha Chelsea na Moses kurudi Chelsea baada ya muda wa mkopo wake kuisha Conte aliamua kwenda na Moses katika mechi za mwanzo wa msimu Pre Season na Moses alitumia nafasi hiyo vizuri kumuonyesha kocha mpya kua bado ana uwezo wa kuichezea klabu ya Chelsea, kocha Antonio Conte akautaarifu uongozi wa Chelsea kua wasimuuze wala kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo kwani alihisi atakua na msaada mkubwa katika kikosi chake na Moses hakumuuangusha kocha wake kwani msimu huu amekua moja ya wachezaji wanaotegemewa sana kwenye kikosi cha Chelsea kitu kilichopelekea kuongezewa mkataba mpya
Tags: Chelea
, New Contract
, Nigeria
, Victor Moses
, Victor Moses sign new contract
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment