Climb the mountains
Champions LeagueChelseaEvertonlukakuLukaku to Chelsea
Chelsea wanaamini watamsajili Lukaku baada ya mshambuliaji huyo kukataa kuongeza mkataba mpya na Everton.
Klabu ya Chelsea ina matumaini ya kumsajili na kumrudisha darajani aliyekua striker wao Romelu Lukaku baada ya nyota huyo kugoma kuongeza mkataba na klabu yake ya Everton,Lukaku amekataa kuongeza mkataba mpya baada ya kuwaambia Everton angependa kucheza ligi ya mabingwa ulaya msimu unaokuja. Chelsea sio klabu pekee inayomfukuzia mshambuliaji huyo kwani klabu ya Manchester United na Arsenal nao wanafuatilia kwa karibu hali ya mchezaji huyo katika klabu yake ya Everton. Chelsea walimuuza Lukaku kwenda Everton baada ya mshambuliaji huyo kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha Chelsea na inasemekana alimshinikiza Jose Mourihno amuuze,hata hivyo mwanzoni mwa msimu huu alinukuliwa akisema atarudi Chelsea kwani kuna mambo ambayo hajamaliza katika klabu ya Chelsea.
Tags: Champions League
, Chelsea
, Everton
, lukaku
, Lukaku to Chelsea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment