Klabu ya Chelsea imekua na matokeo mazuri uwanjani msimu huu ambayo yamewafanya kuongoza ligi kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi 10. Habari nzuri zinaendelea kuingia kwenye klabu ya Chelsea baada ya nyota wake wengi kupanda thamani katika soko la wachezaji na hawa ni wachezaji ambao thamani zao zimepanda sana kwa mwaka 2017
1. DIEGO COSTA (+£68 MILIONI)
Thamani ya sasa: £90 Milioni
Thamani ya awali: £38 Milioni
Diego Costa ndiye mchezaji ambaye thamani yake imepanda Zaidi kwa jumla ya £68 milioni na kufanya thamani yake ya sasa kua £90 milioni,mapema mwezi wa kwanza klabu ya Tianjin Quanjian waliwasilisha ofa yao ya £70 milioni katika klabu ya Chelsea ili wawauzie mchezaji huyo na walikua tayari kumlipa Diego Costa mshahara wa £30 milioni kwa mwaka ofa ambayo ilileta utata kwani tetesi zilidai Diego Costa alisusia mazoezi baada ya Chelsea kukataa ofa hiyo. Kama Chelsea watamuuza mwisho wa msimu bila shaka watatengeneza fedha nzuri.
2. N’GOLO KANTE (+£40 MILIONI)
Thamani ya sasa: £70 Milioni
Thamani ya awali: £30 Milioni
Katika vitu ambavyo klabu ya Leicester City wanajuta hivi sasa ni kumuuza Kante kwa kwa ada ya £30 milioni kwenda Chelsea,tunaweza kusema Kante ni moja ya usajili bora kabisa msimu huu tangu aanze kuichezea klabu ya Chelsea amezidi kuonyesha ubora wake siku baada ya siku,juzi kiungo wa zamani wa Chelsea N’golo Kante alisema anaamini kwa sasa Kante ndiye kiungo bora kabisa barani Ulaya. Kiwango cha Kante kimekua kichocheo kikubwa sana kwenye kupandisha thamani yake kwani ameongezeka £40 milioni na kumfanya kua na thamani ya £70 kwa sasa kitu ambacho kitawaingizia Chelsea pesa nyingi sana kama wataamua kumuuza.
1 3. VICTOR MOSES (+£20 MILIONI)
Thamani yake ya sasa: £30 milioni
Thamani yake ya awali: £10 milioni
Naamini hata Victor Moses yeye mwenyewe hakutegemea kama angekuwa na kiwango cha juu ghafla kama alivyoweza kufanya msimu huu kwani baada ya kutolewa kwa mkopo kwa miaka mitatu mfululizo akienda kwenye klabu kama Liverpool, Stoke City na West Ham United ndoto yake ya kucheza soka ndani ya klabu ya Chelsea ilionekana kama imekufa, ila alichokifanya msimu huu ni mageuzi makubwa na imempelekea kupanda thamani katika soko la wachezaji na kufikia £30 milioni kutoka thamani yake ya awali ya £10 milioni
1 4. PEDRO (+£9 MILIONI)
Thamani ya sasa: £30 Milioni
Thamani ya awali: £21 Milioni
Pedro alijiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2015 akitokea klabu ya Barcelona huku Chelsea wakiwalipa Barcelona £21 milioni ili kukamilisha usajili wake,ilionekana kama Chelsea wamenunua mchezaji mzuri kwa bei rahisi sana kwani katika mechi yake ya kwanza tuu aliweza kufunga goli moja na kutengeneza goli moja. Ila baada yah apo habari ilikua ni tofauti kwani kiwango chake kilishuka sana kiasi cha kuwashangaza hata wachezaji wenzake na wadau wengi wa mpira, zikaenea tetesi kua Pedro angeondoka Chelsea baada ya msimu kuisha ,ila mambo yakageuga baada ya Conte kuchukua timu na kuamua hatamuuza Pedro. Ilikua hamasa kubwa sana kwa Pedro kumlipa fadhila bosi mpya wa Chelsea na mpaka sasa tayari ana magoli 11 msimu huu huku akiwa moja ya wachezaji waliofanikiwa sana na mfumo mpya wa Conte 3-4-3. Kiwango chake kizuri msimu huu kimekuja na matokeo mengi ikiwa pamoja na kupandisha thamani yake sokoni na sasa amefikia thamani y a £30.
1 5. MARCOS ALONSO (+£7 MILIONI)
Thamani ya sasa: £30 Milioni
Thamani ya awali: £23 Milioni
Wakati akisajiliwa na Chelsea kutoka klabu ya Fiorentina kwa ada ya £23 milioni watu wengi walihisi Chelsea wamemsajili mchezaji ambaye sio sahihi wakiamini ni sababu wamekosa wachezaji waliokua wanawafukuzia kwa sababu alisajiliwa masaa machache kabisa kabla ya dirisha la usajili halijafungwa. Baada ya kumsajili Conte alianza kuutumia mfumo wake wa 3-4-3 mfumo ambao unawatumia sana mabeki wanaopandisha mashambulizi (Wing Backs) kuanzia hapo amekua mchezaji mwenye umuhimu mkubwa katika kikosi cha Chelsea kitu kilichofanya kumpandisha thamani yake kutoka £23 milioni mpaka £30 milioni.








No comments:
Post a Comment