Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaDiego CostaEvertonlukakuReal Madrid.Alvaro Morata

Chelsea wapo tayari kumuuza Diego Costa kwa £95 milioni na kisha kuwanunua mafoward hawa.




Gazeti la SunSport limeripoti kocha wa Chelsea Antonio Conte na Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Chelsea Michael Emenalo wamekubaliana kumuuza mshambuliaji wao hatari Diego Costa kwa ada ya £95 milioni mwishoni mwa msimu huu. Wakati wakijiandaa kumuuza nyota huyo wamemtaja Lukaku kama mchezaji wao wa kwanza wanayetegemea kumsajili kuziba nafasi ya Diego Costa huku Alvaro Morata akitajwa kusajiliwa kama mshambuliaji wa akiba,inaaminika kiasi cha £35 milioni kinahitajika kumsajili Morata ambaye thamani yake imeshuka tangu arudi Real Madrid. Emenalo anategemea kiasi cha £60 milioni kitatosha kumsajili Lukaku ambaye zamani alikua mchezaji wa Chelsea kabla ya kuuzwa kwa ada ya £35 milioni kwenda Everton. Conte yupo kwenye mipango wa kujenga kikosi cha muda mrefu katika klabu ya Chelsea na Mkurugenzi wa michezo Emenalo amesema yupo tayari kummuunga mkono kocha huyo kwani wakati akianza kuifundisha Chelsea klabu ilishindwa kukamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji alokua akiwahitaji Zaidi.



No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib