Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Bernardo SilvaChelseaManchester unitedMonaco

Kauli ya Benardo Silva yaziamsha Chelsea na Manchester United.



Kiungo mwenye miaka 22 tuu lakini ni moja ya viungo bora kabisa duniani kwa sasa, Bernardo Silvaanacheza soka katika klabu ya Monaco ni moja ya wachezaji wanaohitajika sana na vilabu vikubwa barani ulaya na anatazamiwa kuondoka klabu ya Monaco mwisho wa msimu huu na Monaco tayari washapanga kiasi cha fedha wanachohitaji ili kumuuza kiungo huyo,wako tayari kumuuza kiungo huyo kwa ada ya £70 milioni. Jana kiungo huyo aliulizwa na waandishi wa habari waliokua wakimuhoji kabla ya mechi yao dhidi ya Manchester City, walimuuliza kuhusu tetesi za kuhusishwa na vilabu vikubwa barani Ulaya alisema “Ni kweli nasikia hizo habari sijui kama ni za kweli au laa ila nina furaha kuhusishwa na timu kubwa ulimwenguni, katika Maisha yangu ya soka ningependa kucheza katika ligi zenye ushindani na ubora wa hali ya juu ningependa sana kucheza ligi ya Uingereza pia naipenda ligi ya Hispania” Kauli hiyo imeziamsha klabu za Chelsea na Manchester United kwani ni klabu ambazo zimekua zikimfuatilia mchezaji huyo tangu akiwa Benefica n ahata alipojiunga na Monaco. Hata hivyo klabu hizo zitalazimika kulipa kiasi cha £70 milioni ili kumpata nyota huyo mdogo anayefanya vizuri barani ulaya.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib