Climb the mountains
ChelseaDiego CostaEden HazardLondon DerbyWest Ham
Chelsea wawachapa West Ham nyumbani kwao sasa kuongoza ligi kwa tofauti ya alama 10.
Chelsea jana waliendeleza kampeni yao ya kuchukua ubingwa wa Uingereza msimu huu baada ya kuwachapa West Ham United goli mbili kwa moja katika uwanja wao wa nyumbani na sasa wanaongoza ligi kwa alama 10 tena kwani juzi baada ya ushindi wa Tottenham walipunguzwa pointi hadi alama 7. Magoli ya mechi ya jana yaliwekwa nyavuni na Eden Hazard aliyemalizia shambulizi zuri la counter attack na goli la pili likifungwa na Diego Costa. Katika Uchaambuzi wa mechi kwanza kabisa inaonekana kiungo Cesc Fabregas ameweza kuitetea nafasi yake ndani ya klabu ya kwani jana alianza mechi yake ya tatu mfululizo baada ya kupitia kipindi kigumu cha kuachwa benchi mara kwa mara kitu kilichopelekea klabu nyingi kumfukuzia ila Cesc yeye mwenyewe akakataa na kuweka wazi kua atapigania nafasi yake Chelsea. Kitu kingine inaonyesha hali ya usalama bado haijaimarika katika mechi ya West Ham dhidi ya Chelsea kwani jana mashabiki wa West Ham walijaribu kuwavamia wachezaji wa Chelsea waliokua wakisheherekea goli la Eden Hazard, katika mechi ya jana klabu ya West Ham iliwazuia mashabiki wake 100 kuingia uwanjani kutokana na vitendo vya uvunjivu wa amani walivyovifanya katika mechi ya Chelsea iliyopita.
Tags: Chelsea
, Diego Costa
, Eden Hazard
, London Derby
, West Ham
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment