Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Antonio ConteChelseaLondon Football AwardsLondon Football Awards 2017

Ujumbe wa Conte kwa mashabiki wa Chelsea baada ya Inter Milan kuweka wazi kua wanataka kumnuna akawe kocha wao.....Nina furaha kua Chelsea


Mapema wiki hii kumekua na habarii kua miamba  wa  Italia Inter Milan wamemtengea dau nono kocha wa Chelsea Antonio Conte ili aweze kujiunga nao huku wakimuahidi kumpa mshahara wa paundi milioni 10 kwa mwaka pamoja na fedha nyingi za usajili kitu ambacho kiliwashtua mashabiki wengi wa Chelsea lakini jana Conte yeye mwenyewe alitoa tamko rasmi. Alipoulizwa kuhusu tetesi zinazo muhusisha na  klabu ya Inter Milan kocha huyo alisema anafuraha na maisha ya Chelsea na hana mpango wa kuondoka hivi karibuni,alisema unapoanza kuifundisha timu mpya kwanza unaijenga jinsi unavyotaka iwe na baada ya hapo unaanza kuangalia kama mbinu zako zimefanikiwa(Akimaanisha yeye bado yupo kwenye hatua ya kujenga timu) huku akisema kuijenga timu ni kitu kinachochukua muda mrefu sana kwani inakubidi ukuze na uendeleze wachezji wako wewe mwenyewe ushinde makombe hapo ndio utaona umejenga timu yenye mafanikio.alipoulizwa kuhusu familia yake kubakia nchini Italia alisema "Kweli kwa sasa familia yangu ipo nyumbani (Italia)ila nategemea na wao watajiunga na mimi siku sio nyingi kwa sababu nawahitaji sana.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib