Climb the mountains
Ceser AzpilicuetaChelseachelsea tanzaniaMarcos AlonsoNemanja matic
Conte: Azpilicueta,Alonso na Matic hawaendi popote.
Baada ya klabu ya Barcelona kuwatuma mascout wake kwenda kuwaangalia wachezaji watatu wa Chelsea wakati wa mchezo dhidi ya West Ham United kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema kua wachezaji hao hawaendi popote. alisema "Ni kawaida wachezaji kuhusishwa na kuhamia vilabu mbali mbali lakini kwangu sioni sababu ya Alonso,Azpilicueta au Matic kuhamia klabu ya Barcelona kwa kigezo cha klabu kubwa duniani kwani klabu ya Chelsea ni kubwa sawa na Barcelona au Real Madrid,nafurahia tunafanya kazi nzuri hapa Chelsea mimi wachezaji wangu na makocha wenzangu na tutaendelea kufanya hivo ila ni kitu cha kawaida timu kufuatilia wachezaji hata kuwaangalia" Alonso na Azpilicueta wamekua na msimu mzuri chini ya kocha Conte wamekua ni moja ya wachezaji waliokibadirisha kikosi cha Chelsea kabisa.
Tags: Ceser Azpilicueta
, Chelsea
, chelsea tanzania
, Marcos Alonso
, Nemanja matic
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment