Climb the mountains
AFC BournemouthChelseaJohn TerryMLSStoke Citywest bromWest Brom want John Terry
West Brom wamesema watajaribu kumsajili John Terry mwisho wa msimu
Kocha wa West Brom Tony Pulis aviambia vyombo vya habari kua klabu yake itajaribu kumsajili John Terry kwa mara ya pili mwishoni mwa msimu baada ya jitihada zao kumsajili wakati wa dirisha dogo kugonga mwamba,Tony Pulis alisema "Nimekua naamini Terry ni moja ya wachezaji bora kabisa kupata kutokea na ni moja ya wachezaji tuliojaribu kuwasajili mwezi January lakini hatukufanikiwa nadhani aliamua kubaki Chelsea kwa sababu wanafukuzia ubingwa wa Uingereza na yeye kwake itakua heshima kama ataondoka akiwa bingwa" Terry ambaye amecheza mechi moja tuu ya ligi kuu tangu mwezi wa 9 mwaka jana mkataba wake unaisha msimu huu hivi karibuni alipofanya mahojiano na chombo kimoja cha habari aliweka wazi kua amekua na ndoto za kucheza ligi ya Marekani kabla hajasataafu kucheza soka la kulipwa. Ukitoa West Brom klabu za Stoke City na Bournemouth ni klabu zinazomfukuzia mkongwe huyo wa Chelsea.
Tags: AFC Bournemouth
, Chelsea
, John Terry
, MLS
, Stoke City
, west brom
, West Brom want John Terry
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment