Climb the mountains
ChelseaChelsea loan playersChelsea loan systemJeremie Boga
Jeremie Boga:Chelsea inatujali sana wachezaji tuliotolewa kwa mkopo,hatujisikii kama tumetupwa.
Jeremei Boga ni moja ya wachezaji 37 ambao klabu ya Chelsea iliwatoa kwa mkopo kwenda kucheza katika klabu nyingine barani ulaya yeye akitolewa kwenda klabu ya Granada inayocheza katika ligi ya Hispania La Liga. Wachezaji wachache ambao Chelsea iliwatoa kwa mkopo wameweza kua tegemeo kwenye timu zao huku wengine wakifanikiwa kurudi Chelsea na kupata namba ya kudumu mfano Thibaut Courtois na Victor Moses ambao kwa sasa ni tegemeo kwenye kikosi cha Conte. Palikua na maneno mengi kuhusu Chelsea kuwatoa wachezaji wengi kwa mkopo wengi wakihoji ni jinsi gani inaweza kuwapatia uangalizi sawa wachezaji wote hao na bado wanunue wachezaji wengine ila Jeremei Boga aliamua kujibu tuhuma hizo akisema Chelsea inawajali sana wachezaji waliotolewa kwa mkopo kwani kila moja anafuatiliwa kwa karibu kabisa na watu wa Chelsea na huwa wanawaangalia kwenye Tv wanavyocheza na wakati mwingine huenda viwanjani na baada ya mechi hizo hupigiwa simu na makocha wa Chelsea ambao huwapatia maelekezo, kuwatumia video za mafunzo na kuwauliza kuhusu maisha yao katika klabu walizowapeleka. Pia alisema wachezaji waliotolewa kwa mkopo wana group lao la WhatsApp ambalo wanatumia kuwasiliana na kutiana moyo ili wafikie malengo yao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment