Kinda wa Chelsea Charlie Wakefield mwenye umri wa miaka 18 aliamua kumshtukiza baba yake ambaye alikua anatimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwa kumpa zawadi ya gari aina Jaguar XE lenye thamani ya £25,000 sawa na milioni 70 za kitanzania. Charlie ni moja ya wachezaji makinda wenye kiwango cha juu kabisa katika academy ya Chelsea akiisaidia Chelsea Under 18 na under 21 kushinda makombe kama FA na UEFA Youth Leagua mara mbili mfululizo alifanikiwa kusaini mkataba wake wakua mchezaji wa kulipwa akiwa na miaka 17 tuu, Charlie alimuelezea baba yake kama mtu muhimu sana katika Maisha yake ya soka kwani hajawahi kukosa kwenda kumuangalia katika mechi hata moja tangu akiwa na miaka 8 na muda mwingine ilimlazimu baba yake kundesha gari kwa masaa 6 ili tuu kwenda kumuangalia akicheza,alisema baba yake alikua akitumia gari aina Ford Focus la mwaka 2003 ambalo alinunua likiwa limeshatumika tayari. Alisema amempa Jaguar kwa sababu ni gari ambalo baba yake amekua na ndoto ya kununua muda mrefu na kwa sasa ndio gari lililokua ndani ya uwezo wake kulinunua.
Climb the mountains
Charlie WakefieldChelseaChelsea Under 18Jaguar XEKinda wa chelsea ampa baba zawadi ya gari
Kinda wa Chelsea amshtukiza baba yake na zawadi ya gari aina ya Jaguar XE lenye thamani ya milioni 70.(PICHA)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment