Akosua Puni Essien ni mke wa aliyekua kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Ghana Michael Essien ameingia katika vichwa vya habari baada ya kuinunua klabu inayoshiriki ligi daraja la tatu nchini Italia FC Como kwa bei ya £206,000 sawa na milioni 560 za Kitanzania. Aliinunua timu hiyo katika mnada wa hadhara baada ya timu hiyo kufirisika hata hivyo ununuzi huo hautahusisha kiwanja cha mazoezi na nembo ya Calciao Como. Fc Como ilikua ikicheza ligi ya Italy Seria B kabla ya kushuka daraja mwisho wa msimMicu na sasa ipo nafasi ya saba katika msimamo wa ligi garaja la tatu. Wakati mke wa Essien akinunua klabu hiyo mume wake alikua nchini Indonesia akisaini mkataba wa kujiunga na klabu ya Persib Bandung ambayo amesaini mkataba wa kuitumikia kwa mwaka moja huku kukiwa na kipengele kitachomuwezesha kuongeza mktaba mwingine.
Climb the mountains
Akosua Puni EssienFC ComoGhanaMichael EssienPersib Bandung
Mke wa Essien anunua timu ya daraja la tatu Italia katika mnada wa hadhara.
Tags: Akosua Puni Essien
, FC Como
, Ghana
, Michael Essien
, Persib Bandung
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment