Wakati kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane akiwa anahangaika kumpata kipa wa kiwango cha kimataifa (World-Class) huku makipa David De Gea na Thibaut Courtois wakiwa chaguo lake la kwanza klabu ya Chelsea imeanza mipango ya kuhakikisha Real Madrid hawamchukui kipa wao ila mipango hiyo inakuja na gharama. Klabu ya Chelsea itatakiwa kumpa Thibaut Courtois mkataba wenye thamani ya £200,000 kwa wiki sawa na milioni 550 za Kitanzania ili kumshawishi nyota huyo kubaki darajani. Kitu ambacho kinawafanya Real Madrid wamuangalie Zaidi Courtois ni sababu ameshawahi kucheza La Liga kwa miaka mitatu akiwa na klabu ya Atletico Madrid na alionyesha kiwango kikubwa kitu kilichowapelekea Chelsea kumrudisha darajani na kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza na kumuuza mkongwe wao Peter Cech.
Climb the mountains
Thibaut CourtoisThibaut Courtois new contractThibaut Courtois to Madrid
Thibaut Courtois bado yupo kwenye rada za Real Madrid Chelsea watatakiwa kumpa mkataba wa £200,000 kwa wiki ili kumbakisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment