Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

EA sportsEA SPORTS N'golo KanteEA SPORTS Player of the SeasonEA SPORTS Player of the Season for 2016/17Kante

Huu ni mwaka wa N'golo Kante...... Ashinda tuzo nyingine tena kutoka kwa EA Sports.


Hakika ule msemo ambao watu wengi wamezoea kujisemea "Huu ni mwaka wangu" umekua kweli kwa mchezaji wa Chelsea N'golo Kante ambaye amekua kwenye kiwango bora kabisa msimu huu pamoja Chelsea kuchukua ubingwa lakini Kante ameweza kuchukua tuzo nne za peke yake zote zikiwa ni tuzo za mchezaji bora wa msimu wa 2016/2017. Mapema leo asubuhi kampuni ya EA Sports inayotengeneza michezo mbali mbali ya kompyuta (Games) moja wapo ukiwa Fifa imemtangaza Kante kama mshindi wa tuzo yao ya mchezaji bora wa mwaka, Kante aliipokea tuzo hiyo na kusema "Ni heshima kubwa sana kwangu kuchaguliwa na taasisi zenye majina makubwa kwenye mpira na nataka kuwashukuru wote walionipigia kura" aliendelea kusema " ninafanya mazoezi kwa juhudi kubwa sana ninapokua mazoezini pia ninajitahidi kuonyesha juhudi uwanjani nikiwa na wachezaji wenzangu wenye uwezo wa juu ambao kwa pamoja tumeweza kushinda kombe la ligi"

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib